HARMONIZE ATOA USHAURI KWA WASANII - DJ Makiss Music - New Songs Download HARMONIZE ATOA USHAURI KWA WASANII

HARMONIZE ATOA USHAURI KWA WASANII

HARMONIZE ATOA USHAURI KWA WASANII

HARMONIZE ATOA USHAURI KWA WASANII 


Msanii Harmonize amewasihi wasanii kuutumia miziki Singeli kuimba masuala ya kijamii vitu vya maana zaidi ili kuuongezea thamani na kuufanya muziki huo uwe wa kusikilizwa na rika zote pasipo kubaguliwa na kundi fulani kutokana na ujumbe unaokuwa umeimbwa na msanii husika?


Harmonize ametoa ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo mbali na hilo Konde alifichua kuwa anatarajia kuachia ngoma mbili za kimataifa (International Bangers) usiku mmoja ndani ya mwezi Julai, ambapo atawashirikisha wasanii wengine wawili wakubwa ambao hakuwaweka wazi.


Singeli umekuwa ni miongoni mwa muziki pendwa nchini kwa sasa, Ikumbukwe Julai 3 tulishuhudia Mfalme wa Bongo Flava Alikiba akiachia wimbo wake wa kwanza wa Singeli (Ubuyu) ngoma ambayo sio tu kutoa burudani ni ngoma inayokemea tabia zisizofaa kutoka kwa watu, jamii na rika mbalimbali.

Post a Comment

أحدث أقدم