Msanii wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria, Burna Boy ameweka wazi matamanio yake ya kufanya shoo ya bure Burkina Faso mwishoni mwa mwaka huu.
Burna ameweka wazi matamanio hayo kupitia ukurasa wa Instagram wa No Of Weakness Tv ambao ni ukurasa rasmi wa kutangaza maoni yake yanayotarajiwa kutoka kati ya Mei au Juni mwaka huu.
Burna amesema kama itawezekana atafurahia kuwapa watu wa Burkina Faso burudani ya bure kabla ya mwaka huu kuisha.
"Kama itawezekana itakuwa jambo la heshima kuwapa watu wa Burkina Faso shoo ya bure muda fulani mwaka huu kabla ya kumalizika Inshaallah," ameandika.
Burna Boy hutoza dola milioni 1 zaidi ya sh2 bilioni kwa onyesho moja. Lakini endapo onesho hilo litafanyika pesa zitakazopatikana zitatolewa kwa Rais Ibrahim Traore ili kusaidia katika shughuli za matumizi ya nchi hiyo.
Hatahivyo mastaa wakubwa Afrika wakivutiwa na uongozi wa Ibrahimu Traore mfano Sarkodie, Stefflondon, na sasa ni Burna Boy ambaye ameenda mbali zaidi na kutaka kuwapa burudani bure watu nchini Burkina Faso.
0 Comments