Maua Sama azua gumzo, Je Ni Kweli au Kuna Jambo Jipya?
Msanii wa Bongo Fleva nchini, Maua Sama, amezua maswali kadhaa kwa mashabiki wake kuhusu kile alichokiandika katika ukurasa wake wa Instagram kuhusu suala zima la mapenzi kwa upande wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Maua Sama amesema kuwa ni muda sasa anapitia hali isiyo nzuri katika mahusiano yake, lakini haoni matumaini ya kupendwa tena.
"Habari za Muda huu mashabiki zangu ,ndugu na marafiki ni muda sasa napitia kati hali isiyo nzuri kwenye mahusiano yangu,(toxic relationship).Nawekeza muda mwingi kumpenda mtu Nampa kila kitu na lakini sioni matumaini ya kupendwa . Sijawahi kuwafungukia kuhusu mahusiano yangu ila inafika pahala nanyoosha mikono juu …!! SIWEZI TENA" aliandika Maua Sama.
Sasa Wadau mpaka hivi sasa wanaulizana, je ni kweli hali hiyo inamkuta Maua Sama Kiuhalisia, ama kuna kazi mpya Inakuja?
إرسال تعليق