Msanii Yammi Rasimi aachwa na lebo ya African princess inayomilikiwa na Nandy
African Princess Records inapenda kuwataarifu rasmi wadau wa muziki, vyombo vya habari, na mashabiki wote kuwa msanii wetu mpendwa Yasirun Yasin Shaban, anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii Yammi, amehitimisha rasmi mkataba wa mkataba wa kazi zake na lebo yetu ya The African Princess Label kwa makubaliano ya kirafiki na manufaa ya pande zote mbili.
Katika kipindi chake akiwa chini ya The African Princess Label, Yammi ameweza kung'ara na kuonyesha kipaji kikubwa kilichowavutia wengine ndani na nje ya Tanzania.
Tumeshuhudia mafanikio makubwa kupitia nyimbo zilizofanya vizuri, maonyesho ya moja kwa moja (live performances), na ukuaji wa umaarufu wake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
Tunaamini kuwa lebo imetoa mazingira bora yaliyomwezesha Yammi kukua na kupevuka kisanaa, na tunafurahia kuona kuwa sasa amepata wapya waliovu-tiwa maoni na zaidi kipaji chake na kumsaidia hatua kubwa zaidi kimataifa.
Kuondoka kwake pia kutoa nafasi kwa African Princess Records kuendelea na dhamira yake ya kuwainua wasanii wapya, kuwekeza kwao, kuendelea kuchangia katika maendeleo ya muziki wa Tanzania na Afrika.
Tunamtakia Yammi kila la heri katika safari yake mpya ya muziki. Ataendelea kuwa sehemu ya familia ya African Princess, na mafanikio yake yatabaki kuwa sehemu ya historia yetu ya mafanikio ya pamoja.
Imetolewa na:
Uongozi
ikoni Princess Records
yeye: 05/05/2025
0 Comments