Msanii Davido amzawadia dola 5000 shabiki yake aitwaye Ananzo
Mkali huyo wa Afrobeat kutoka Nigeria, David Adeleke 'Davido' amemzawadia shabiki wake aitwaye Ananzo, dola 5000 baada ya kucheza wimbo wake 'With You' aliomshirikisha Omah Lay kutoka kwenye filamu yake ya 5ive.
Ananzo ambaye ni TikToker wa Ghana baada ya kufanya challenge ya wimbo huo wimbo, ilifanya Davido amzawadie dola 5000 sawa na Sh12 milioni.
Albamu ya 5ive nyimbo 17 ikijumuisha With You ft Omah Lay ilitoka Aprili 18, 2025 ikiwa yenye thamani ya tano kutoka kwa Davido imekuwa na mafanikio makubwa tangu kuachiwa kwake, ikiongoza kwa kusikiliza kupitia majukwa mbalimbali ya kidijitali.
Utakumbuka, kitendo hicho cha Davido kumzawadia shabiki huyo pesa kimekuja siku chache baada ya msanii huyo kumzawadia mkewe 'Chioma' gari jipya aina ya G-wagon AMG G63 katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake akitimiza miaka 30. Pia Davido alimpa muuzaji wa gari hilo dola 10,000 sawa na sh 269 milioni.
Hata hivyo Chioma inaonekana mwenye furaha kiasi cha kutokwa na machozi wakati akikabidhiwa zawadi ya gari kwenye tafrija ya siku ya kuzaliwa ambayo mwimbaji huyo alimuandalia.
Ni wazi kwamba Davido si mgeni wa kufanya ukarimu kwa watu wake. Mnamo Novemba 2021, alichangisha Naira milioni 200 kupitia kampeni ya mitandao ya kijamii na kuongeza naira milioni 50 ya fedha zake mwenyewe, kwa ajili ya vituo 292 vya watoto yatima Nigeria.
Pia, Julai 2023 aliendelea na utamaduni huo kwa kuchingia naira milioni 237 kwenye vituo 424 vya watoto yatima na kunufaisha zaidi ya watoto 13,000.
Kama haitoshi Novemba 2024, aliahidi naira milioni 300 kusaidia vituo vya watoto yatima na kutumia mabaya ya dawa za kulevya kwa vijana.
Mnamo 2018, alitoa naira milioni 15 kwa ajili ya upasuaji wa lugha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed, Nigeria.
0 Comments