Msanii Rich Mavoko ametoa Neno kuhusu Ibraah
Msanii wa mziki wa bongo fleva kutokea nchini Tanzania Rich Mavoko ametoa maoni yake kuhusiana na sakata linaloendelea hivi sasa kumuhusu Ibraah na boss wake Harmonize.
Nikukumbushe siku chache nyuma msanii Ibraah alitangaza kuwa anataka kutoka kwenye label yake lakini changamoto ni kwamba boss wake Harmonize amemuambia alipe bilionioni moja ndo atoke na kwawakati huu yeye kipato chake hakiruhusu,hivyo Ibraah akaamua kuchangisha michango .
Mapema hivi leo Rich Mavoko amesema kuwa kwa wakati huu ni muda wake msanii Ibraah atulize akili iliaweze kufanya kitu sahihi.
'niseme huu ni wakati mzuri lakini pia ni wakati mbaya kwake muhimu atulize akili ili aweze kufeel the pain ambayo anayo ,Alisema Rich Mavoko
0 Comments