Harmonize aeleza sakata la Ibraah na kukiri kwamba hajamdai Ibraah shilingi bilioni moja kama alivyodai
C.E.O na Mwanzilishi wa Konde Gang, Staa wa Bongofleva Harmonize amejirekodi video fupi akielezea sakata hilo na kukiri kwamba hajamdai Ibraah shilingi bilioni moja kama alivyodai.
Nikiri kwamba Mdogo wangu alinitumia msg na kuniomba kwamba anataka kutoka kwenye Label na kwenda kujitegemea nami nilimjibu moja kwa moja kwamba nakutakia kila la kheri, kaa chini na Viongozi wa Konde Gang soma mkataba wako muone mnafanyaje, mkataba unasema endapo atataka kuvunja mkataba na kumiliki nyimbo zote hata zile alizozifanya na mimi ili ziwe zake milele ziwe zinaingiza kwake inatakiwa alipie hicho kiasi cha pesa kilichotajwa miaka minne iliyopita
Hayo ndio yalikuwa mazungumzo sijui nini kimetokea kwake baadae akaja kusema kwenye mitandao yake kwamba nimemdai kiasi cha shilingi BILIONI MOJA, nikiri kwamba sijamdai kiasi cha BILIONI MOJA na nisingependa pesa yangu tena ije kunichafua mwenyewe, namtakia kila la kheri, kuanzia sasa yeye ni Msanii anayejitegemea Promoters mkiwa na show muiteni apate rizki aisaidie familia yake
Kuhusu kauli yake ya kusema kwamba nilimuita chumbani, kwamba nimemwambia amtoe Mama yake Mzazi inahuzunisha, sina namna Mtoto akiunyea mkono huwezi kuukata, nimemuachia Mungu, nimemsamehe na ninamuombea, sihitaji msamaha wowote kutoka kwake akiona kuna tija sawa, akiona kuna haja ya kuomba msamaha Watu waliosikia maneno hayo ni sawa lakini anayestahili kuombwa msamaha zaidi ni Mwenyenzi Mungu ameongea Harmonize
0 Comments