Abigal Chams ameandika historia kwa kuonekana kwenye jalada la toleo la Mei la jarida la Rolling Stone Africa
Abigal Chams ameandika historia kwa kuonekana kwenye jalada la toleo la Mei la jarida la Rolling Stone Africa, ambapo amepewa jina la utambulisho: Future of Music Abigail Chams.
Abigail Chams Steps Into The Light From soulful strings to Swahili lyrics, Abigail Chams invites listeners into a soundscape where tradition meets innovation, wameandika kwenye Instagram baada ya kushare cover lake.
Rolling Stone limemwelezea Abigail kama msanii wa kipekee mwenye mafunzo ya muziki wa kitaalamu, akitambuliwa kwa uwezo wake wa kupiga vyombo vitano vya muziki pamoja na ustadi wa lugha tatu: Kiingereza, Kiswahili na Kifaransa.
Sauti yake ni mchanganyiko wa kuvutia wa mitindo mbalimbali ikiwemo Afro RnB, Bongo Flava, Taarab na Amapiano, na yote haya yameonyeshwa kwa ustadi katika EP yake ya kwanza ya mwaka 2023 iitwayo 5.
Baada ya kutoa wimbo mmoja tu, Abigail alisainiwa na Sony Music Africa mwaka 2022, na tangu hapo safari yake ya muziki imekuwa ya kasi na ya kipekee.
Wimbo wake wa hivi karibuni, Me Too akiwa amemshirikisha Harmonize, umeelezewa kama hatua kubwa ya kimuziki ukiambatana na uzalishaji wa hali ya juu na sauti tamu ya Abigail inayobeba hisia za kina na ukomavu wa kiusanii.
Abigail pia amevunja rekodi kwa kuwa msanii wa kike wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuteuliwa kwenye Tuzo za BET, hatua inayodhihirisha kuwa anaelekea mbali zaidi katika muziki wa kimataifa.
0 Comments