New AUDIO | AliKiba - Ubuyu Msanii Alikiba Achia kionjo cha wimbo wa Singeli | Download - DJ Makiss Music - New Songs Download

New AUDIO | AliKiba - Ubuyu Msanii Alikiba Achia kionjo cha wimbo wa Singeli | Download

Asante kwa shauku yako katika Makiss Music, mahali pako salama pa kusambaza muziki wako. Tunathamini maswali, maoni na maswali yako Jisikie huru kuwasiliana nasi kupitia njia zifuatazo Usaidizi kwa Wateja WhatsApp +255718308551 Chat ya Moja kwa Moja Inapatikana kwenye tovuti yetu saa za kazi

New AUDIO | AliKiba  - Ubuyu Msanii Alikiba Achia kionjo cha wimbo wa Singeli | Download 


Moja ya kitu ambacho kilikuwa kinasubiriwa kwa hamu kwenye muziki wa Tanzania ni kumuona msanii mkongwe, anayependwa, na mwenye ushawishi mkubwa kwenye tasnia hiyo, Ali Salehe Kiba Alikiba akifanya muziki wa Singeli ambao ndio nembo ya nchi hii inayotambulika Kimataifa kwasasa.


Alikiba ambaye anaheshimika kama Mfalme wa Bongo Fleva, yupo mbioni kuachia wimbo wake wa kwanza wa Singeli, aina ya muziki ambayo inawakilisha mitaa ya jiji la Dar es Salaam, na kusambaa sehemu mbalimbali za dunia.


Hivi karibuni, Kiba ameachia kionjo cha wimbo huo utakaofahamika kama Ubuyu, ujio wake huo hauashirii tu mageuzi yake binafsi kama msanii, bali unaashiria wakati muhimu kwa muziki wa Singeli na mafanikio makubwa kwa muziki wa Tanzania.


Hatua hii ya kimkakati ya mmoja wa wasanii mashuhuri zaidi wa Afrika Mashariki inaweza kuunda upya mipaka ya muziki, na kuinua sauti za wasanii wachanga wa muziki huo katika hatua kubwa zaidi.


Umuhimu wa jina “Ubuyu” na maana yake ya kitamaduni

Jina la "Ubuyu" lina mguso na maana kubwa Kitamaduni hapa Tanzania ambayo inatokana na lugha ya Kiswahili, neno hilo likimaanisha uvumi au porojo tamu, kwa lugha nyepesi wenyeji huita umbea, Kwa kuchagua jina hili, Alikiba anagusa kipengele kinachohusiana na maisha ya kijamii ya kila siku ya Mtanzania.



Post a Comment

0 Comments