Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz amezua mjadala mitandaoni mara baada ya kushea baadhi ya picha zake na kuzisindikiza na wimbo wa Ibraah "Copy &Paste"
Burudani Wakati Sakata la ibraah tz na Waajiri wake ambao ni lebo ya Muziki ya kondegang likiendelea kushika kasi na kufikia hatua ya kupeana maonyo makali na kutaka kushtakiana Mahakamani
Maswali yamekuwa ni mengi je, Diamond anampango wa kumsaini Msanii huyo baada ya kuachana na Waajiri wake Au Anajikumbushia yaliyowahi kutokea kati yake na Harmonize wakati alipotaka kutoka kwenye lebo ya WCB
Wimbo wa Copy and Paste una tafsiri tofauti tofauti yamkini Diamond anamaanisha yaliyotokea kipindi kile wakati lebo ya WCB ilipomtaka Harmonize kulipa Milioni 600 kuondoka kwenye lebo hiyo na kuona kuwa ni uonevu, sasa Harmonize ameyafanya kwa Ibraah kwa kumtaka alipe Bilioni 1 (copy & paste).
Je, we Unadhani Diamond anamaana gani kutumia wimbo huu?
0 Comments