Jay Melody Ametangaza ujio wa Album yake Mpya
msanii wa Bongo Fleva, Jay Melody ametangaza ujio wa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la "Addiction". Akieleza hisia zake za kipekee juu ya muziki, Jay Melody ameandika Kupitia ukurasa wake wa Instagram:
"Dear music, thanks for always clearing my head, healing my heart, and lifting my spirits. Music is my Addiction."
Akiambatanisha ujumbe huo wa kugusa moyo na hashtag addictionthealbum, msanii huyo pia amethibitisha kuwa albamu hiyo itatoka rasmi tarehe 9 Mei 2025 – akiwataka mashabiki wake "kuhifadhi tarehe"
Hii ni albamu ya pili kutoka kwa Jay Melody baada ya Therapy kuibuka moja ya kazi bora zaidi mwaka jana, ikipokelewa kwa shangwe na mashabiki ndani na nje ya Tanzania.
0 Comments