Barnaba ametangaza rasimi kuachia wimbo mpya na diamond platnumz inaitwa Salama
Baada ya takriban miaka mitatu kupita tangu walipokutana kwenye wimbo "Hadithi" uliokuwa sehemu ya barnabaclassic – Love Sounds Different, sasa wasanii hawa wakali wa Bongo Fleva wamerudi tena na kazi mpya!
Wimbo wa Hadithi unaendelea kufanya vizuri hadi leo, ukiwa na maoni zaidi ya milioni 10 kwenye YouTube.
Leo Barnaba ametangaza rasmi kuwa kesho asubuhi mapema, atadondosha kolabo mpya kabisa na diamondplatnumz inayoitwa Salama.
Jitayarishe! Inakaribia kuwa hit nyingine kuu!
0 Comments